24 Oktoba 2016 - 18:12
Halifa wa Daesh akimbia mji wa Musol kukimbilia katika mipaka ya Syria na Iraq

Kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh (Abubakari Al Baghdadiy) amekimbia mji wa Musol nchini Iraq pamoja na familia yake, akiwa na jeshi la watu 50 wakielekea katika mipaka ya Iraq na Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: gazeti moja la Lebanon limeandika kuwa Abubakari Al baghdadiy kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh akiwa na familia yake, huku akiongozwa na wanajeshi 50 katika magaidi wa Daesh katika mji wa Musol amekimbia mji huo wakielekea katika mipaka ya Syria na Iraq.
Gazeti la Annahar likinukuu kutoka katika vyanzo vya ulinzi nchini Iraq limeandika kuwa: shambulizi la jana la kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Rabtiyah magharibi mwa Iraq, yalikuwa na malengo ya kuficha hatua ya kutoroka kwa kiongozi mkuu wa kikundi hicho kutoka katika mji huo kwenda sehemu ya mipaka ya Syria na Iraq.
Majeshi ya Iraq yamevizingira vijiji 8 viliopo kaskazini mwa mashariki mwa Iraq ambapo kutoka sehemu vijiji hivyo kuna umbali wa kilometa 9 mpaka kufika katika mji wa Musol ambapo ndio inadaiwa kuwa makao makuu ya serikali ya magaidi hao.
Shirika la UNICEF limetangaza kuwa mpaka sasa kuna watoto 600 elfu katika mji wa Musol ambao hawana hali nzuri na wanahitajia msaada wa haraka katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
mwisho wa Habari/290